Published On:Jumamosi, 13 Septemba 2014
Posted by Hisia
NI MUHIMU KUMTANDIKA MARCIO MAXIMO KESHO NGAO YA JAMII - JOSEPH OMOG
Kocha wa Azam fc, Joseph Omog (katikati)
NI MECHI MUHIMU! Kocha mkuu wa
klabu ya Azam Joseph Marius Omog ameutaja mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii
dhidi ya Yanga kuwa ni mchezo muhimu.
Omog amesema ni muhimu kwa timu yake kushinda
mchezo wa kesho ili kuimarisha Morali ya timu kabla ya kuanza kwa ligi.
Azam inacheza mchezo huu kwa mwaka wa tatu
mtawalia ambapo miaka miwili ya nyuma ilikua inacheza kama makamu bingwa na
mara zote ilipoteza dhidi ya mabingwa Simba na Yanga, kesho inacheza kama
bingwa kwahiyo Azam ina nafasi kubwa kushinda kama historia itatenda haki
lakini pia kutokana na maandalizi na usajili uliofanyika.
Raia huyo wa Cameroun alisema amewapa wachezaji wake kilakitu kitakachowawezesha kushinda mchezo huo, Kwahyo kazi imebaki kwao kushinda na kuleta furaha klabuni.