Published On:Jumamosi, 13 Septemba 2014
Posted by Hisia
SHINJI KAGAWA ARUDISHA MAKALI, AIPIGIA MOJA BORUSSIA DORTMUND
Shinji Kagawa akishangilia baada ya kuifungia Borussia Dortmund bao tangu arudi klabuni hapo
SHINJI Kagawa amefurahia ndoto za kurudi
Bundesliga kufuatia kiungo huyo wa zamani wa Manchester United kufunga
bao moja na kutengeneza moja katika mechi yake ya pili akiichezea
Borussia Dortmund.
Nyota huyo wa kimataifa wa Japan,
alimtengenezea Adrian Ramos bao lake la kwanza katika dakika ya 34 dhidi
ya Freiburg, kabla ya kufunga la pili kabla ya mapumziko.
Kagawa alikaribishwa vizuri ambapo alisalimiwa na mabango na bendera za Japan.
Nyota wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa (kulia) akishangilia bao lake katika uwanja wa Westfallonstadion