Published On:Jumatatu, 8 Septemba 2014
Posted by Hisia
Maximo amegonga penyewe - Niyonzima
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kocha wake Mbrazili, Marcio Maximo, hakukosea kumbadili namba.
Maximo amembadili namba Niyonzima kutoka kwenye namba nane aliyoizoea kuicheza hadi namba 11.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema anaimudu vilivyo namba hiyo na kocha Maximo hakukosea kumbadili kwa kuwa ndiyo anayoitumia akiwa katika timu yake ya taifa ya Amavubi ya Rwanda.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema anaimudu vilivyo namba hiyo na kocha Maximo hakukosea kumbadili kwa kuwa ndiyo anayoitumia akiwa katika timu yake ya taifa ya Amavubi ya Rwanda.
“Ukiwa mchezaji unatakiwa ujue namba nyingi za kucheza, hivyo ndivyo
ilivyo kwa upande wangu, nipo fiti na najua namba nyingi uwanjani
tofauti na hii.
“Kocha Maximo hakukosea kunibadili namba kwa kuwa ndiyo namba
ninayoitumia nikiwa katika timu ya taifa na ninaimudu kwa kufanya
vyema.“Naamini nitafanya vyema msimu ujao kwenye ligi nikiwa katika
namba yangu hiyo mpya na ninaamini tutatwaa ubingwa,” alisema Niyonzima.
Hata hivyo, Maximo alifunguka kuwa ameamua kumbadili namba mchezaji
huyo kutokana na kasi aliyonayo ili aweze kusaidia kutoa pasi nzuri kwa
wenzake, iwe rahisi katika suala zima la ufungaji.